County
Mkuu wa Polisi Matuga Aaga Dunia
Afisa mkuu wa Polisi eneo la Matuga kaunti ya Kwale William Cheruiyot Koros ameaga dunia.
Idara ya usalama katika kaunti ya Kwale imethibitisha kutokea kwa kifo chake, japo haijatoa taarifa kamili kuhusu sababu zilizopelekea afisa huyo kuaga dunia kwani mapema leo ameonekana kutekeleza majukumu yake ya kikazi kama kawaida.
Kamanda wa Polisi kaunti ya Kwale Reginald Omario amesema afisa huyo wa polisi amethibitishwa kuaga dunia na maafisa wa afya baada ya kuanguka na kukimbizwa hospitalini.
Omario amesema maafisa wa kiafya tayari wameanzisha uchunguzi kubaini kilichosababisha kifo chake kisha idara ya polisi itatoa taarifa kamili kwa umma kwani mwili wa marehemu umesafirisha jijini Nairobi.