Business

Wavuvi kaunti ya Kwale walalamikia kutohusishwa kwa vikao vya umma

Published

on

Baadhi ya Wavuvi katika kaunti ya Kwale wamelalamikia hatua iliyochukuwa na kamati ya ukusanyaji maoni ya umma kuhusu mswada wa usimamizi na maendeleo ya uvuvi.

Wavuvi hao walieleza kwamba hawakuhusishwa kikamilifu katika ukusanyaji wa maoni hivyo basi hali hiyo huenda ikaathiri matakwa ya wavuvi na jamii zinazotegemea uvuvi.
Aidha waliitaja hatua hiyo kuwa ukiukaji wa haki zao za kikatiba kwani kamati hiyo ilipaswa kuwaelimisha na kuwapa nakala za mswada huo ili waweze kutoa mapendekezo yao.
Wakati huo huo waliitaka kamati hiyo kurejelea zoezi hilo kwa njia mbadala ili kuhakikisha kila mwananchi anapata nafasi ya kuelewa na kujadili vipengele muhimu vya mswada huo kabla ya kutoa maoni yao
Taarifa ya Mwanahabari wetu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version