News

Jamii ya Digo kaunti ya Kwale yakosoa serikali kuhusu MRC

Published

on

Jamii ya wadigo katika kaunti ya Kwale imejitokeza na kuikosoa serikali dhidi ya kauli yake kwamba kuna tetesi za kuzuka kwa vuguvugu la Mombasa Repubilican Council MRC.

Jamii hiyo ikiongozwa na Balozi Chirau Ali Mwakwere ilisema kauli hiyo ya serikali inalenga kuchangia uzushi na wasiwasi kwa jamii hiyo, kwani kuna njama za kuzuka kwa vuguvugu la MRC.

Balozi Mwakwere, alisema jamii ya wadigo haiungi mkono vuguvugu la MRC na iwapo serikali iko na taarifa zozote kuhusu kauli hizo basi iwaeleze wananchi ili wafahamu na wala sio kuchangia uzushi na wasiwasi kwani kauli hizo huenda zikaathiri sekta ya utalii.

“Tulishangaa kabisa kusikia serikali ikisema hivyo kwa sababu huo ni uzushi na imetutia wasiwasi sana kwenye familia zetu, watoto wetu, sisi wazee, wake kwa waume, kwa sababu hakuna MRC hiyo iliisha zamani, sasa serikali inasema imeanza tena, twaiomba serikali itwambie imeanza tena ni akina nani?”,aliuliza Mwakwere.

Jamii hiyo hata hivyo iliweka wazi kwamba haitakubali kuhusishwa na makundi ambayo hayana msingi wowote kwa wananchi.

“Mwataka kutwambai sisi wanawake wa Kidigo twazaa visirani? Sisi hatujazaa visirani, ielekeweke hivyo hatujazaa na wala hatutazaa visirani. Sisi kama kama magen z wa hapa ndani ya Kwale hatukufanya vurugu la aina yeyote leo tunakuaje sisi ni MRC au kwa sababu sisi niwanyonge?”,walisema wakaazi hao.

Kauli zao zilijiri baada ya serikali kupitia kaunti ya kamishna wa kaunti ya Kwale Stephen Orinde kusema kwamba kuna taarifa za kijasusi za kuchipuka kwa vuguvugu la kundi la MRC ambalo linalenga kutatizo usalama wa kaunti ya Kwale.

Taarifa ya Joseph Jira

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version