Business
Wavuvi Kwale wadai kuhangaishwa na wavuvi wa Tanzania
Wavuvi kaunti ya Kwale walalamikia kukandamizwa na wavuvi kutoka taifa jirani la Tanzania kufuatia mizozo ya mipaka.
Kulingana nao wavuvi hao, wamekua wakinyanyaswa na hata kutozwa faini ya hadi shilingi milioni 4 wanapopatikana wakivua katika sehemu zinazodaiwa kuwa katika nchi ya Tanzania na maafisa hao.
Juma Rama Yusuf mwenyekiti wa wavuvi eneo la Jimbo na mwenzake wa Vanga Ngoto Mohamed walisema kuwa wavuvi wa Tanzania wamepewa uhuru wa kutekeleza shughuli za uvuvi humu nchini ili hali wenyeji wanahangaika.
Aidha waliitaka serikali ya Kenya na ile ya Tanzania kuja pamoja na kutatua swala la mipaka katika bahari hindi ili kukomesha mizozo ya mara kwa mara inaoshuhudiwa kati ya wavuvi wa Kenya na maafisa walinda bahari kutoka Tanzania.
Taarifa ya Pauline Mwango