News

Kindiki, aendeleza mpango wa Wezesha jamii Taveta

Published

on

Naibu Rais Prof Kithure Kindiki ameahidi kuendeleza mpango wa Wezesha jamii maarufu Economic Empowerment Programme maeneo mbalimbali kote nchini.

Akizunguza katika kaunti ya Taita taveta wakati wa halfa hiyo, Kindiki amesema serikali itahakikisha wananchi wanakabiliana na changamoto mbalimbali za kiuchumi nchini.

Kindiki ambaye aliambatana na viongozi wengine wa Kenya Kwanza, akiwemo mbunge wa Kapseret Osacar Sudi wameushtumu upande wa upinzani wakisema hawana ajenda maalum.

Waziri wa madini na raslimali za baharini nchini Ali Hasan Joho alieleza azma yake ya kuwania wadhfa wa urais ifikapo mwaka 2032 huku akisema kwamba ana imani kwamba rais Ruto atahudumu kwa mihula miwili.

Kwa upande wake Kimani Ichungwa ambaye ni mbunge wa Kikuyu na kiongozi wa walio wengi katika bunge la kitaifa alisema hatua ya Wezesha jamii ni njia moja wapo ya kufanikisha ajenda ya rais ya kuinua mwananchi wa chini.

“Hii mambo ya Empowerment mnaona tukifanya ni moja wapo ya ajenda na ahadi ya rais William Ruto katika mpango mzima wa Bottom Up, huyo mama wa chini aweze kupata pesa ya kufanya biashara hivyo sisi tumeamua wapige kelele wasipige, waseme tunawahonga wakenya hiyo sio shida yetu sisi tunataka kuona yule mwananchi wa chini anafaidika ndani ya serikali ya Rais William Ruto”. Alisema Ichung’wah.

Wakaazi wa Taveta katika mkutano wa Wezesha jamii

Hata hivyo siasa za rais Ruto kuhudumu mihula miwili zilisheheni huku viongozi mbalimbali wakitoa hundi za fedha ili kufanikisha mradi huo wa Wezesha jamii.

Miongoni mwa viongozi ambao walihudhuria halfa hiyo ni pamoja na Spika wa bunge la kitaifa Moses Wetangula, Spika wa bunge la Seneti Amason Jeffa Kingi, Waziri wa michezo Salim Mvurya, Waziri wa madini na raslimali za baharini Ali Hassan Joho.

Taarifa ya Elizabeth Mwende

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version