News
Mudavadi: Mazungumzo yanaendelea kuhusu mzozo wa Kenya na Tanzania
Mzozo kati ya Kenya na Tanzania umeanza kutokota kufuatia ilani iliyotolewa siku ya Jumanne Julia 29, na serikili ya Muungano wa Jumhuri ya Tanzania.
Serikali hiyo ya Tanzania kupitia Waziri wa Biashara na viwanda nchini humo Selemani Jefo ilitoa ilani ya kuwazuia wafanyibiashara wa kigeni kuendelea kufanya baadhi ya biashara katika taifa hilo.
Kutokana na hilo, Waziri wa masuala ya kigeni nchini Musalia Mudavadi alisema juhudi zimeanza za kuishawishi serikali ya Tanzania kuondoa vikwanzo hivyo na kwamba Rais William Ruto anafanya mazungumzo na mwenzake wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kuhusu suala hilo.
“Rais William Ruto ambaye ni Mwenyekiti wa Jumaiya ya Afrika Mashariki anafanya mazungumzo na rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan na mwafaka utapatikana kwani pia suala la diplomasia ni mwafaka na hii tatizo tutatua kama serikali kupitia mazungumzo ya kidiplomasia”, alisema Mudavadi.
Kwa upande wake Waziri wa biashara na viwanda nchini Lei Kinyanjua alionya kwamba huenda serikali ya Kenya ikachukua hatua sawa na hiyo dhidi ya Tanzania iwapo taifa hilo la Afrika Mashariki halitaangazia upya vikwanzo hivyo.
Mzozo huo wa kidiplomasia umejiri siku moja tu baada ya Waziri wa biashara na viwanda nchini Tanzania Selemani Jafo kutangaza kwamba serikali ya Tanzania imepiga marufuku wafanyibiashara wa kigeni dhidi ya kufanya biashara ndogo ndogo nchini humu ili kuruhusu watanzania kujiimarisha kiuchumi.
Taarifa ya Mwahoka Mtsumi