News

Mahakama ya Kilifi yaanzisha upya kesi ya ulaghai wa pesa

Published

on

Mahakama ya Kilifi imeanzisha upya kesi ya mwanaume mmoja anayekabiliwa na shtaka la ulaghai wa pesa.

Hii ni baada ya Mwanaume huyo kwa jina Samuel Ngonyo, kuachiliwa kwa dhamana hapo awali lakini alikosa kudhuhuria vikao Mahakamani hali iliyopelekea kesi hiyo kuanzishwa upya.

Hakimu mkuu wa Mahakama hiyo Charles Obulutsa aliagiza jamaa huyo kuzuliwa rumande baada ya agizo la kukamatwa kwake kuidhinishwa na Mahakama baada ya jamaa huyo kupuuza vikao vya Mahakama vya awali.

Kabla ya agizo hilo, Mahakama ilielezwa kwamba mnamo tarehe tofauti kati ya mwezi Septemba hadi Oktoba mwaka 2021 katika maeneo la Ganze kaunti ya Kilifi kwa kutumia njia ya ulaghai, mshukiwa alichukua pesa taslimu shilingi elfu 50 ya mlalamishi Grace Sidi Katana.

Mahakama ilielezwa zaidi kwamba mshukiwa alitekeleza kitendo hicho baada kumdanganya Mlalamishi kwamba yeye ni Mwandishi na afisa wa kazi za umma hivyo angemsaidia Moses Katana mtoto wa mlalamishi kupata kazi ya serikali.

Kesi hiyo itaendelea mnamo tarehe 13 mwezi Agosti mwaka huu.

Taarifa ya Mwanahabari wetu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version