News

KEBS, Yawaonya Wananchi Kuhusu Bidhaa Ghushi

Published

on

Shirika la kutathmini ubora wa bidhaa nchini KEBS limesema wakenya wengi wamekuwa wakinunua bidhaa ghushi ambazo hazijathibitishwa na Shirika hilo kutokana na ukosefu wa ufahamu kuhusu ubora wa bidhaa.

Shirika hilo ambalo limeandaa warsha ya siku moja na Wanahabari mjini Kilifi, kuelezea hatua zilizopigwa na Shirika hilo katika kukabiliana na bidhaa ghushi nchini, limesema juhudi hizo zitaendelezwa ili kuhakikisha bidhaa zimeafikia viwango hitajika.

Shirika hilo pia limetoa wito kwa wakenya kuwa waangalifu wanaponunua bidhaa mbalimbali kutoka kwa maduka au sokoni ili kuepuka kuuziwa bidhaa ghushi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version