Rais Ruto apigania mageuzi katika sheria ya ukuaji wa Afrika-(AGOA)

Rais Ruto apigania mageuzi katika sheria ya ukuaji wa Afrika-(AGOA)

Rais William Ruto amesema Kenya na Marekani zitasaini mkataba wa kibiashara ifikapo mwisho wa mwaka huu.

Rais Ruto anatarajiwa pia kushinikiza Washington kuongeza mkataba wake wa kutotozwa ushuru na Afrika kwa angalau miaka mitano.

Akizungumza pembezoni mwa mkutano wa kila mwaka wa baraza kuu la umoja wa mataifa mjini New York nchini Marekani, rais Ruto alidokeza mipango ya kukutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio baadaye, ili kujadili sheria ya fursa ya ukuaji wa afrika (AGOA).

Sheria hiyo iliyodumu kwa miaka 25, inatoa fursa kwa mataifa ya Afrika yanayohitimu kutotozwa ushuru wa kibiashara katika soko la Marekani, na inatazamiwa kamilika mwezi huu.

Kiongozi wa taifa alisema anaamini kuwa utawala wa Marekani umeongeza uthamini wake kwa AGOA.

Taarifa ya Joseph Jira