Serikali kuongeza mshahara wa maafisa wa polisi kwa asilimia 40

Serikali kuongeza mshahara wa maafisa wa polisi kwa asilimia 40

Katibu katika Wizara ya usalama wa ndani Raymond Omollo ametangaza nyongeza ya asilimia 40 kwa mishahara ya maafisa wa polisi ambayo itaanza kutekelezwa mwezi Julai mwaka huu.

Omollo ambaye anaongoza Kamati maalum ya kuangazia mishahara na marupurupu ya maafisa wa polisi nchini, alisema pendekezo lililowasilishwa kwa hazina ya kitaifa, afisa wa kiwango cha chini kabisa wa polisi atapokea shilingi 57, 700 kutoka shilingi 38,975.

Pendekezo hilo pia linataka afisa wa chini kabisa wa idara ya magereza kupokea kiwango cha shilingi 57,700 huku Afisa wa polisi aliyefuzu kutoka chuo cha Kiganjo akipendekezwa kupokea mshahara wa shilingi 29,296 kutoka shilingi 20,390.

Hata hivyo afisi wa kiwango cha chini kabisa kutoka Shirika la huduma kwa vijana wa taifa NYS atapokea mshahara wa shilingi elfu 26 huku afisa wa NYS wajuu zaidi akipokea mshahara wa shilingi elfu 37.

Pendekezo hilo pia limeafikia kwamba maafisa wa polisi wa ngazi ya juu zaidi watalipwa kati ya shilingi 301,548 na shilingi 584,903 ikiwa ni nyongeza ya asilimia ya juu zaidi.

Wakati huo huo Inspekta Jenerali wa Polisi nchini Douglas Kenja amesema hatua hiyo inalenga kuhakikisha maafisa wa polisi wanatekeleza majukumu yao vyema huku Afisa mkuu mtendaji wa Tume ya maadili na kupambana na ufisadi nchini EACC Abdi Ahmed Mohamud akiwarai maafisa wa polisi kujiepusha na ufisadi.

Taraifa ya Mwahoka Mtsumi