Rais Samia aitisha mazungumzo na upinzani

Rais Samia aitisha mazungumzo na upinzani

Rais wa Tanzania Samia Suluhu sasa ametaka mazungumzo na upinzani wa taifa hilo baada ya uchaguzi uliokumbwa na utata na ghasia.

Wito huu ukitolewa siku moja baada ya kukamatwa kwa katibu mkuu wa chama cha upinzani cha CHADEMA Amani Golugwa kwenye msako wa kuwatafuta washukiwa wa ghasia za baada ya uchaguzi.

Emmanuel Nchimbi ambaye ni makamu wa rais wa Tanzania alisema hatua hiyo ni kutoa fursa kwa wapinzani kusikizwa na kuhakikisha Tanzania inasalia yenye amani.

Nchimbi alisema rais Samia Suluhu Hassan anania ya kuweka udhabiti wa taifa hilo sawa na kuweka mazingira bora kwa wawekezaji.

Rais Samia amekosolewa pakubwa kutokana na uchaguzi huo ulioshuhudia kuzimwa kwa mitindao pamoja na kukandamizwa kwa vyombo vya habari.

Waangazili wa mashirika kama vile umoja wa afrika, na hata muungano wa mataifa ya kusini mwa afrika SADC yalisema uchaguzi huo haukuwa huru na haki.

Taarifa ya Joseph Jira