Tume ya uchaguzi ya Tanzania INEC yazima ndoto ya Luhaga Mpina

Tume ya uchaguzi ya Tanzania INEC yazima ndoto ya Luhaga Mpina

Tume huru ya uchaguzi nchini Tanzania (INEC) imekiandikia chama cha upinzani cha ACT Wazalendo kuwa hakitaweza kumteua mgombea wa urais kupitia chama hicho, Luhaga Mpina.

Katika barua ambayo INEC imeiandikia ACT-Wazalendo, tume hiyo ya uchaguzi ilirejea uamuzi wa Ofisi ya msajili wa vyama vya siasa uliotolewa siku ya Jumatano Agosti 27, 2025 ambao ulisema mgombea wa urais wa chama hicho Luhaga Mpina, hakukidhi matakwa ya Katiba na kanuni za ACT kuwania nafasi hiyo.

ACT-Wazalendo walipokea barau kutoka kwa msajili wa vyama vya kisiasa kujieleza jinsi ilivyoendesha mchakato wa kumpata mgombea wake wa urais kama yalivyokuwa madai ya mwanachama wa chama hicho, Manalisa Ndala.

Barua hiyo ya INEC ilihitimisha kwa kueleza kwamba inafuta barua yake ya Agosti 15,2025 kuhusu urejeshaji wa fomu kwa mgombea na kumtaka asifike katika ofisi hizo kwa ajili ya uteuzi.

Hata hivyo, chama cha ACT-Wazalendo kilisema kwenye taarifa yake kwamba kinaupinga uamuzi wa Ofisi ya majili na pia kilisema Tume ya uchaguzi ilijiongoza vibaya kwenye kukubaliana na kile uchaguzi mkuu Tanzania kufanyika Oktoba 29.

Chama cha ACT- Wazalenzo kilishikilia kwamba maagizo ya msajili mkuu wa vyama vya kisiasa ni kinyume na matakwa ya kikatiba yanayoitangaza Tume hiyo kuwa ni huru na isiyochukuwa amri kutoka chombo chochote kile.

Katika taarifa hiyo, Katibu mkuu wa chama hicho, Ado Shaibu, aliiomba Tume ya Uchaguzi kubadilisha uamuzi wake na kutokuifanya ionekane kutokuwa huru kwenye utekelezaji wa kazi zake kisheria.

Hata hivyo mgombea wa urais wa chama cha CCM, Samia Suluhu Hassan na chama cha upinzani cha NRA, Hassan Kisabya Almas, walikamilisha hatua ya uteuzi na kukabidhiwa magari aina ya Landcruiser ambayo watayatumia katika kampeni zao za uchaguzi zinazotarajia kuzinduliwa.

Taarifa ya Mwahoka Mtsumi