Sports
Harambee Stars Yajiondoa CECAFA
Timu ya taifa ya soka ya Kenya, Harambee Stars, imejiondoa rasmi katika michuano ya CECAFA inayojumuisha mataifa manne: Tanzania, Kenya, Uganda na Senegal, ambayo yalipangwa kufanyika Karatu, Arusha, nchini Tanzania.
Uamuzi huo umetolewa na kocha mkuu wa Harambee Stars, Benni McCarthy, kwa kushirikiana na kamati ya kiufundi, wakieleza wasiwasi wao kuhusu ubora wa viwanja vya mazoezi pamoja na uwanja wa kuandalia mechi hizo.
Michuano hiyo inatarajiwa kuanza rasmi leo, ambapo Harambee Stars ilikuwa imepangiwa kufungua pazia kwa kuvaana na wenyeji, Taifa Stars ya Tanzania.
Shirikisho la Soka nchini Kenya (FKF), kupitia barua rasmi kwa vyombo vya habari, limethibitisha taarifa hizo.
Michuano hiyo ilikuwa sehemu ya maandalizi ya timu shiriki kuelekea mashindano ya CHAN, ambayo yanatarajiwa kuanza rasmi katika kipindi cha siku 12 zijazo.