Sports

Gor Yatimua Benchi La Kiufundi na Afisa Mkuu Mtendaji Wake

Published

on

Kilabu ya Gor Mahia imevunjiliwa mbali kamati yake ya kiufundi ikiongozwa na kocha mkuu Zedekia ‘Zico’ Otieno kufuatia msimu mbovu wakiambulia patupu.

Mabingwa hao mara 21 wametaja hatua hiyo kuwa ni ya kujenga upya Kogalo baada kupoteza ligi ya taifa FKF kwa kilabu ya Kenya Police.

Wakufunzi washikilizi hao yani Otieno na Nam walipewa nafasi ya kunoa kogalo kwa muda baada ya kilabu hiyo kumtimua Raia wa Croatia Sinica Mihic kutokana na msururu wa matokeo duni.

Ni mara ya kwanza Kogalo kukosa kushiriki kimataifa huku nafasi hizo zikitwaliwa na Police ambao watashiriki ligi ya mabingwa barani Afrika CAF champions ligi na Nairobi United tajia la mashirikisho Barani Afrika CAF confederation.

Vile vile Mabingwa hao wazamani walitengaza kuachana na Afisa mkuu mtendaji Ray Oruo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version