Sports
Barcelona Yamkabidhi Jezi Namba 10 Kwa Lamine Yamal
Kilabu ya FC Barcelona imemkabidhi winga matata Lamine Yamal jezi namba 10 kilabuni humo.
Jezi hilo ambalo limevaliwa na baadhi ya wakongwe kilabuni humo ikiwemo Lionel Messi na Ronaldinho imekua na kiungo Ansu Fati ambaye kwa sasa ameondoka kilabuni humo na kujiunga na Monaco ya Ufaransa.
Huku hayo yakijiri kilabu hiyo imekumbwa na wasiwasi kuhusiana na tabia ya winga huyo katika msimu huu mapumziko baada ya kanda kumuonyesha akijivinjari na mpenzi mwenye umri mkubwa na pia ukaribu wake na Neymar wakionekana maeneo tofauti wakijivinjari mpaka saa za usiku.
Mchezaji Huyo mwenye umri wa miaka 19 alijiunga na Timu hiyo kutoka kwenye Akademia ya Kilabu hiyo LA MASIA na amekua nguzo muhimu chini ya kocha Hansi Flick akiongeza kilabu hiyo kushinda taji la Laliga na Copa De La Rey.