News

Debora: Serikali kuu imepiga hatua katika upanzi wa miti nchini

Published

on

Waziri wa mazingira nchini Debora Mulongo alisema serikali kuu imepiga hatua katika upanzi wa miti nchini.

Mulongo alisema wizara hiyo inalenga kuhamasisha wananfunzi kote nchini kukumbatia zoezi la upanzi wa miti ili kuimarisha mazingira.

Kulingana na Mulongo ni muhimu kwa wanafunzi wa shule mbalimbali nchini kuhusishwa ili nao pia wachangia katika upanzi wa miti nchini na kuafikia azma ya serikali ya kupanda miti bilioni 15 ifikipo mwaka wa 2032.

‘’Ni lazima kila Mkenya alichukulie suala la upanzi wa miti kwa uzito ili kuimarisha mazingira ya hapa nchini Kenya’’, alisema Mulongo

Waziri Mulongo, akipanda miti na wananchi.

Waziri Mulongo alisema kufikia sasa takribani miti milioni 800 imepandwa na akawataka Wakenya kuwa mstari wa mbele katika upanzi wa miti ili kuchangia katika udhibiti wa athari za mabadiliko ya tabianchi.

Taarifa ya Janet Mumbi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version