News

Chibule, awahimiza wakaazi kuzingatia uhifadhi wa mazingira

Published

on

Naibu Gavana wa kaunti ya Kilifi Flora Mbetsa Chibule, aliwahimiza wenyeji wa kaunti ya Kilifi kuwa mstari wa mbele kukabiliana na uchafuzi wa mazingira.

Akizungumza wakati wa Maadhimisho ya siku ya Mazingira duniani yalifanyika siku ya Alhamisi tarehe 5 Juni, 2025, katika uwanja wa Karisa Maitha mjini Kilifi kaunti ya Kilifi, Chibule alisema hamasa zinapaswa kutolewa kwa wanafunzi kuhusu umuhimu wa kutunza mazingira.

Aidha alisisitiza haja ya jamii kuzingatia usafi wa mazingira ili kuzuia mkurupuko wa magonjwa mbalimbali ya kuambukiza.

“Kuna haja ya wazazi pamoja na walimu kuweka mikakati ya kuwaelimisha watoto umuhimu wa utunzaji mazingira na sio kuachia Mashirika na wadau wa mazingira jukumu hili” Alisema Chibule.

Naibu Gavana wa Kilifi Flora Mbetsa Chibule akipamba miti

Vilevile, Chibule alisema watalii wamekuwa wakizuru kaunti ya Kilifi kutokana na mazingira safi na kushinikiza uchakataji wa chupa za plastiki.

Hafla hiyo ambayo ilihudhuriwa na Viongozi mbalimbali pamoja na wadau wa mazingira walitoa wito swa serikali ya kaunti ya Kilifi kutenga kipande cha ardhi ambacho kitatumika kwa utupaji wa taka za plastiki.

Taarifa ya Janet Mumbi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version