Sports
Aldrine Kibet Kujiunga Rasmi Na Celta Vigo Ya Uhispania
Kiungo wa Harambee Stars chipukizi marufu kama Junior Stars Aldrine Kibet sasa ni rasmi anajiunga na kilabu ya Celta Vigo inayoshiriki ligi ya Laliga msimu ujao baada ya wazazi wake kusafiri kuelekea uhispania kukamilisha dili hiyo ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19.
Kibet ambaye alitoka shule ya Upili ya St.Anthony ya Kitale alijiunga rasmi na Akademia ya Nasty mwaka jana ambapo amepata ufanisi mkubwa mno pamoja na beki Amos Wanjala.
Mchezaji huyo mbunifu amewakilisha Junior Stars katika mashindano ya CECAFA na kombe la Bara Afrika mjini Cairo Misri mwezi Mei mwaka huu.
Mchanaji huyo awali na sasa bado ana imani ya kuchezea kilabu ya Barcelona na kuwa mkenya wa kwanza kuchezea mwabingwa hao wa Uhispania.