Sports
Inter Wapiga Msamba, PSG Wakivuma Uefa.
Klabu ya Paris Saint-Germain (PSG) ndio mabingwa wa Klabu bingwa Uropa baada ya kuilaza Inter-Milan magoli 5-0 Jumamosi usiku, katika fainali iliyochezewa katika uwanja wa Allianz Arena jijini Munich, Ujerumani.
Mvua ya magoli ilianzishwa na beki Ashram Hakimi dakika ya 12, kabla ya kiungo mshambuliaji wa PSG Desire Doue kuongeza bao la pili dakika ya 20, na goli la tatu katika dakika ya 60 huku goli la nne na tano likifungwa katika dakika ya 73 na 86 mtawalia.
Kocha wa PSG Luis Enrique amewasifia wachezaji wake sawa na mashabiki waliojitokeza kuishangilia klabu hiyo, ikijipatia taji kuu la kwanza Uropa baada ya kuingia fainali ya mashindano haya mara mbili kwa kipindi cha miaka mitano.
“Nafurahia sana ushindi huu” Alisema Kocha Enrique. “Fainali imekua na hisia sana hasa nilipoona bango la mashabiki kuhusu familia yangu”
Kikosi hichi changa cha PSG kimeafikia kile ambacho wachezaji nyota kama Lionell Messi, Neymar, Zlatan Ibrahimovich, Beckam na Kylian Mbappe walishindwa kutekeleza wakivalia jezi ya PSG
Paris Saint-Germain (PSG) imekua klabu ya pili Ufaransa kushinda taji la Klabu bingwa Uropa baada ya Marseille mwaka 1993.