Entertainment

Ullulations! Sister Shanniez Afunga Ndoa Mtwapa

Drumrolls tafadhali! 🔔🎉 Mtangazaji mahiri wa Coco FM, Sister Shanniez, hatimaye ametoka soko rasmi! Harusi ya kifahari ya kimyakimya, katikati ya jiji la Mtwapa, imegeuza Jumamosi kuwa sinema ya mapenzi ya Pwani. Wageni wachache lakini mashuhuri, vibes za Coco, na miondoko ya kimahaba—ni kama movie, lakini real life! 💍✨”

Published

on

Mtangazaji mahiri wa Coco FM, Sister Shanniez, ameanza ukurasa mpya wa maisha kwa kufunga ndoa katika harusi ya kifahari lakini ya faragha, iliyofanyika Jumamosi Mei 31, katikati mwa jiji la Mtwapa, kaunti ya Kilifi.

Harusi hiyo, iliyosheheni uzuri wa Pwani na mvuto wa mazingira ya kimahaba, ilifanyika kwa mwaliko maalum kwa watu wa karibu tu.

Miongoni mwa waliohudhuria walikuwa ni jamaa wa familia, marafiki wa karibu pamoja na baadhi ya wafanyakazi wenzake kutoka Coco FM, waliokuja kushuhudia tukio hilo la kihistoria kwa ukaribu na heshima .

Watangazaji waliokuwa miongoni mwa wageni maalum ni Hamisi Kombe, Mamaa Madikodiko, Teddy Mwanamgambo, Hon Baba Yaga, Kassim Mbui, Binti Umazi, Sifa na Patrick. Uwepo wao katika sherehe hiyo ulidhihirisha mshikamano na urafiki wa kweli uliopo ndani ya familia ya redio hiyo.

Sister Shanniez, anayefahamika kwa sauti yake yenye mvuto na ucheshi wa kipekee hewani kupitia kipindi cha Coco Drive kinachorushwa kila Jumatatu hadi Ijumaa, ameendelea kuwa mfano wa mwanamke jasiri na mwenye msimamo maishani. Mbali na umahiri wake kitaaluma, harusi yake imefungua ukurasa mpya unaodhihirisha utu uzima na maamuzi ya busara katika maisha binafsi.

Kinachovutia zaidi ni kuwa maandalizi na taarifa kuhusu harusi hiyo yalisalia kuwa siri kubwa hadi siku yenyewe ya tukio. Ukimya huo wa kimakusudi ulitoa nafasi ya sherehe hiyo kufanyika kwa utulivu, upendo na heshima ya kipekee, bila minong’ono wala mkorogo wa hadhara.

Ingawa bado hakujatolewa taarifa rasmi kutoka kwake kuhusu tukio hilo, waliokuwepo wameelezea harusi hiyo kama yenye haiba, hisia, na ladha ya mapenzi ya kweli. Tangu kuwasili kwa bibi harusi hadi kwenye mankuli, kila hatua ilikuwa ya kipekee na ya kupendeza.

Ni wazi na dhahiri kuwa sura mpya ya maisha yake ya ndoa inaleta mvuto mpya katika safari yake ya maisha ya ndani na nje ya taaluma yake.

Hapa COCO FM tunasema kila lenye Kheri dada Shanniez na Mwenyezi Mungu akujalie mema kwenye ukurasa huu mpya wa maisha ya ndoa, Amen🙏🏼

2 Comments

  1. Asha kassim

    May 31, 2025 at 9:02 pm

    Congratulations my fave Mungu akujalie kheri njema katika ndoa Yako as your biggest fan am proud of you dear we love you so much 💕💕💕💖💖🫂🫂🫶🫶🫶

  2. Aisha

    June 1, 2025 at 7:39 pm

    Pongezi dada sister shanniz.
    Karibu ndani yake tukaendeshe

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version