News

Mahakama Yaahirisha uamuzi wa Kesi ya Kawi ya Mawe, Lamu

Published

on

Mahakama ya Ardhi na Mazingira mjini Malindi imeahirisha uamuzi wa kesi ya kupinga mradi wa Kawi ya Mawe katika kisiwa cha Amu kaunti ya Lamu.

Mahakama imesema kwamba uamuzi wa kesi hiyo utatolewa mnamo tarehe 30 mwezi Septemba mwaka huu iwapo mradi huo unafaa kutekelezwa katika kisiwa cha Amu au la.

Wakaazi wa kaunti ya Lamu kwa ushirikiano na Shirika la kijamii Save Lamu pamoja na Wanaharakati wengine wa kijamii, wamedai kwamba hawatarudi nyuma hadi haki ipatikane.

Wakaazi hao, wameweka wazi kwamba japo hawapingi mradi wa maendeleo, lakini mradi huo uko na madhara mengi ya kiafya, utaathiri mazingira, utaharibi uchumi wa kaunti sawa na kuangamiza viumbe hai wa baharini.

Kesi hiyo ambayo imekuwa Mahakamani tangu mwaka wa 2019 imekuwa ikipingwa na baadhi ya waekezaji ikiwemo wale wa mradi huo wa Kawi ya Mawe ambao ni Lamu Coal Plant Power.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version