News

Rais Ruto Awaomba Radhi Watanzania.

Published

on

Rais William Ruto amejitokeza na kuomba msamaha kwa niaba ya vijana wa Gen Z dhidi ya utawala wa Serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania.

Rais Ruto ameisihi serikali ya Tanzania kuondoa hofu kuhusu Mabishano makali ya Mtandaoni baina ya mataifa  haya mawili  licha ya Viongozi wa mataifa haya mawili Rais William Ruto na Mwenzake wa Tanzania Samia Suluhu Hassan  kuonekana kujaribu kuuzima moto wa mashambulio ya mitandaoni hasa miongoni mwa vijana wa Gen Z.

Akizungumza wakati wa dhifa ya asubuhi ya maombi ya kitaifa yaliondaliwa jijini Nairobi, Rais Ruto amesema kuna haja ya kuendeleza ushirikiano mwema wa kidiplomasia na wala sio kuchangia uhasama, akiwaomba msamaha pia vijana wakenya.

Viongozi wahudhuria dhifa ya asubuhi ya maombi ya kitaifa

Kauli ya Rais Ruto imejiri baada Bunge la Tanzania kulazimika  kusitisha vikao vya kawaida na kujadili hoja inayotajwa kugusia usalama wa taifa la Tanzania huku wakimpongeza rais Samia Suluhu Hassan kwa hatua aliyochukua ya kuwafurusha Wanaharakati  wa kutetea haki za binadamu wakiongozwa na Martha Karua ambaye kiongozi wa chama cha People’s Liberation Party nchini Kenya na Jaji Mkuu mstaafu Willy Mutunga, Mwanaharakati Boniface Mwangi wa Kenya na Agather Atuhaire wa Uganda.

Mwanaharakati Bonifance Mwangi alipatikana  katika eneo la mpakani mwaka Kenya na Tanzania katika eneo la Lunga lunga ilihali mwenzake  Agather Atuhaire akipatikana karibu na kituo cha mpakani na Mtukula.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version