Sports

Mancity Inamnyemelea Kiungo Tijjani Reijnders

Published

on

Kilabu ya Manchseter City iko kwenye mazungumzo ya moja kwa moja na kiungo wa AC Milani Tijjani Reijnders kumleta ugani Etihad msimu ujao.

Mawakala wa mchezaji huyo wanataka kitita cha pauni milioni 60 kumwachilia mholanzi huyo ambaye amefunga magoli 19 katika mechi 104 ambazo amechezea Milan

Hata hivyo city wako tayari kutoa pauni milioni 55 kupata sahihi yake  na kumpa kandarasi nono mkataba wa miaka mitano ugani Etihad.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 alijiunga na Milan msimu jana akitokea AZ Alkamar ya Eredivise.

City wangali sokoni kupata mrithi wa kiungo mbunifu Kevin De Bruyne ambaye ameondoka kwenye kilabu hiyo baada ya mafanikio makubwa ikidaiwa pia wanamfukuzia kiungo wa Lyon Ryan Cherki raia wa Ufaransa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version