News
Rais Ruto Awaomba Radhi Watanzania.

Rais William Ruto amejitokeza na kuomba msamaha kwa niaba ya vijana wa Gen Z dhidi ya utawala wa Serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania.
Rais Ruto ameisihi serikali ya Tanzania kuondoa hofu kuhusu Mabishano makali ya Mtandaoni baina ya mataifa haya mawili licha ya Viongozi wa mataifa haya mawili Rais William Ruto na Mwenzake wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kuonekana kujaribu kuuzima moto wa mashambulio ya mitandaoni hasa miongoni mwa vijana wa Gen Z.
Akizungumza wakati wa dhifa ya asubuhi ya maombi ya kitaifa yaliondaliwa jijini Nairobi, Rais Ruto amesema kuna haja ya kuendeleza ushirikiano mwema wa kidiplomasia na wala sio kuchangia uhasama, akiwaomba msamaha pia vijana wakenya.
Viongozi wahudhuria dhifa ya asubuhi ya maombi ya kitaifa
Kauli ya Rais Ruto imejiri baada Bunge la Tanzania kulazimika kusitisha vikao vya kawaida na kujadili hoja inayotajwa kugusia usalama wa taifa la Tanzania huku wakimpongeza rais Samia Suluhu Hassan kwa hatua aliyochukua ya kuwafurusha Wanaharakati wa kutetea haki za binadamu wakiongozwa na Martha Karua ambaye kiongozi wa chama cha People’s Liberation Party nchini Kenya na Jaji Mkuu mstaafu Willy Mutunga, Mwanaharakati Boniface Mwangi wa Kenya na Agather Atuhaire wa Uganda.
Mwanaharakati Bonifance Mwangi alipatikana katika eneo la mpakani mwaka Kenya na Tanzania katika eneo la Lunga lunga ilihali mwenzake Agather Atuhaire akipatikana karibu na kituo cha mpakani na Mtukula.
News
Kilabu Ya Liverpool Yamnasa Frimpong

Beki wa kilabu ya Bayern Leverkusen Jeremie Frimpong ni rasmi amejiunga na mabingwa wa ligi kuu Uingereza Liverpool.
Beki huyo mholanzi amejiunga na The Reds kwa pauni milioni 29.5 na amemwaga wino mkataba wa miaka 5 na kilabu hio kuchukua nafasi ya Alexander Trent Arnaold ambaye ni rasmi amejiunga na kilabu ya Real Madrid.
Mholanzi huyo anakua mchezaji wa tano kuvalia jezi ya kilabu hio wengine akiwa ni pamoja na Cody Gakpo,Virgil Van Dijik,Ryan Gravenberch.
Nyota huyo ambaye pia amekuwa akiwindwa na Manchester United na miamba wa Uhispania Rea Madrid amesema kwamba alichagua kilabu hiyo kwani ndio inaendana na mipango yake ya mbeleni kama mchezaji akiahidi kushinda mataji na miamba hao wa Uingereza.
News
Shughuli za Masomo Zatatizwa katika Shule ya Msingi ya Arabuko Sokoke

Shughuli za masomo katika shule ya msingi ya Arabuko Sokoke eneo la Kakuyuni kaunti ya Kilifi zilitatizika mapema siku ya Ijumaa baada ya Wazazi kuandamana wakilalamikia usimamizi mbaya wa shule hiyo.
Wakaazi hao wamemtaka Mwalimu kuu wa shule hiyo kupewa uhamisho kwani ameonyesha wazi kushindwa kusimamia shughuli za masomo katika shule hiyo.
Wakiongozwa na Joyce Mbuche, Wazazi hao wamesema Mwalimu mkuu wa shule hiyo amekosa kuwa wazi kwa wazazi kuhusu suala la matumizi ya Fedha ya shule hiyo pamoja na kutokuwa muadilifu kazini.
Wazazi hao hata hivyo wamesema Mwalimu mkuu huyo amekuwa hawalipi mishahara walimu ambao wanasimamiwa na wazazi katika shule hiyo huku baadhi ya wanafunzi wakikosa kusajiliwa katika mfumo wa KEMIS.