News

Manusua wa Mkasa Baharini, Kilifi

Published

on

Mafisa wa uokoaji kaunti ya Kilifi bado wanaendelea kupiga mbizi baharini kutafuta Mwili wa Mwanabaharia mmoja Kapteni Kivondi, aliyezama Jumamosi usiki wa tarehe 24 Aprili, akiwa na wengine wawili katika mkono wa Bahari mjini Kilifi.

Kapteni Kivondi alifariki pamoja na mwenzake Kapteni Mwidini wakati wa mkasa huo, huku baharia mwengine wa tatu Aisha Jumwa akinusurika baada ya kuogelea baharini kwa zaidi ya masaa 16.

Akizungumza na CocoFm iliyomtembelea Hospitalini mjini Kilifi, Jumwa alielezea matukio hayo wakati mawimbi makali yalipopiga chombo chao na kukizamisha.

Mwili wa baharia mwengine ambaye alikuwa msaidizi wa nahodha wa Dau hilo, Kapteni Mwidini ulipatikana katika ufuo wa Watamu, umbali wa kilomita 50 kutoka mji wa Kilifi. Mwili wa marehemu uliondolewa na kusafirishwa hadi eneo la Likoni Mjini Mombasa kwa Maziko.

Aisha Jumwa -Manusuru wa mkasa wa baharini mjini Kilifi

Jumwa anasema kuwa aliweza kuokolewa siku iliyofuatia ya Jumapili, mwendo was saa sita adhuhuri baada ya kuogelea kwa maasaa hayo 16 licha ya upepo na mawimbi makali yaliyozidi kumsukuma maji makuu.

Kisa hiki kilitokea masaa machache tu hata baada ya idara ya Utabiri wa hali ya hewa kutoa tahadhari ya kuchafuka kwa Bahari na marufuku ya kuepuka fuo za bahari.

Hata hivyo Jumwa anasema kuwa tahadhari hiyo iliwapata kuchelewa hadi mkasa huo ulipowakuta. Anaongeza kwamba baada ya Dau lao kuzama watatu hao walijifunga Kamba ili waweza kuolea na kusaidiana lakini wawili hao wakashindwa na nguvu ya mawimbi hayo makali na kuaga dunia mikononi mwake

Taarifa ya Lolani Kalu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version