Sports
Arsenal Mbioni Kumpata Mshambulizi Sesko
Kilabu ya Arsenal imeambiwa ni lazima itoe kitita cha pauni milioni 75 kunasa huduma za mshambulizi wa taifa la Slovenia na kilabu ya RB Leipzig Benjamin Sesko.
Inaaminika na The Gunners kupitia kwa Afisa mkuu mtendaji Andrea Berta wamekua na mazungumzo ya moja kwa moja na wakala wa mchezaji huyo na pia afisa wa Leipzig Marcel Schafer kuhusiana matakwa ya uhamisho huo.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 alikua na magoli 21 msimu huu akichangia mengine sita katika michezo yote alizoshirikisha akiwa miongoni mwa wafungaji bora ligi ya Bundesliga nchini Ujerumani.
The Gunners wako sokoni kusaka mshambulizi atakayewapa taji msimu ujao huku ikidaiwa pia watafanya mazungumzo na mshambulizi wa Sporting Lisbon Victor Gyokeres ambaye alifunga zaidi ya magoli 40 msimu ambao umekamilika.