News
Kenya Kuandaa Mashindano Ya Karate JKA Mwaka 2027
Kenya imechaguliwa kuandaa mashindano ya mchezo wa Karate wa mabingwa barani Africa wa shirikisho la Japan Karate Association JKA mwaka 2027.
Hii ni mara ya kwanza kabisa mchezo huo kuandaliwa nje ya ardhi ya Africa Kusini.
Rais wa shirikisho la JKA nchini Kenya Wakili George Kithi anasema, hii ni heshima kubwa kwa Kenya kuwa mwenyeji wa mashindano hayo ya kimatifa, na kuongeza Kwamba ni dhihirisho mchezo huu unazidi kupata umaarufu sio tu kwa mashabiki wa Karate nchini Kenya, bali kote barani Africa.

Rais wa shirikisho la mchezo wa karate la Japan Karate Association (JKA) nchini Kenya Wakili George Kithi akiwa na kikosi cha Kenya katika ukumbi wa Ellis Park mjini Johannesberg, Afrika Kusini baada ya kukamilika kwa mashindano ya mwaka huu.
Wakili Kithi anasema, hii itakuwa fursa nzuri Kenya kuonyesha umahiri wake wa kuandaa mashindano ya kimatifa lakini pia kukuza vipawa na kuitangaza Kenya kama kituo Bora Cha Utalii.
Hii inafuatia ushindi mkubwa wakati wa mashindano yaliyokamilika hivi majuzi nchini Africa Kusini ambapo Kenya ilimaliza katika nafasi ya pili nyuma ya Africa Kusini.