News

Vijana wa Kaunti ya Kilifi Wajisajili kwa Kazi za Ughaibuni

Published

on

Mamia ya vijana wamejitokeza katika uwanja wa Karisa Maitha mjini Kilifi Kaunti ya Kilifi kutafuta usajili wa kazi za ughaibuni kama ilivyotangazwa na serikali.

Kulingana na serikali, eneo la Pwani limetengewa nafasi 3,500 za kazi za ughaibuni katika mpango wa ajira uliopewa jina “Kazi Majuu” ikiwepo kazi za kuendesha piki piki, ubawabu, vijakazi shambani pamoja na wahudumu nyumbani.

Wengi wa vijana waliojitokeza katika zoezi hilo wameeleza matumaini ya kubadili maisha yao iwapo watafanikiwa, wakidai maisha ya humu nchini yamezidi kuwa magumu.

Kulingana na Jilani Justin Mwarumba mmoja wa vijana hao wameasema serikali inafaa kuwahakikishia usalama wa pesa watakazotumia katika zoezi hilo huku wakishinikiza kuangazia upya suala la ulipaji mkopo kwa wasio na uwezo wa kugharamia zoezi hilo la usajali.

Hata hivyo Wanaharakati wa kijamii mjini Kilifi wakiongozwa na Birya Menza wanashinikiza serikali kuhakikisha inabuni nafasi za ajira hapa nchini badala ya mataifa ya ugaibuni ambako wakenya wengi wamekuwa wakipitia madhila mengi mikononi mwa waajiri.

Zoezi hilo litaendelea katika kaunti zaMombasa na Kwale.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version