News

Waasi wa M23 wazidisha Mapambano, DRC

Published

on

Mapigano mapya yamezuka mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo baada ya Waasi wa kundi la M23 kufutilia mbali pendekezo la ahadi za hapo awali za kujiondoa katika maeneo wanayoyadhibiti huku wakilishtumu jeshi la Kongo kwa kuendeleza uchokozi.

Wakati hayo yakiarifiwa, mataifa jirani yanaendelea kijaribu kufufua mchakato wa kutafuta amani katika taifa hilo ambalo limetumbukia katika migogogo ya kiutawala. Inaarifiwa kwamba Watu wawili wameuawa kufuatia mashambulio yaliyotokea katika hafla ya Mazishi ya Mwanamuziki maarufu wa Kongo.

Waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda katika maeneo ya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wanapambana na waasi wanaoegemea upande wa serikali huku nchi za kikanda zikijaribu kuupa msukumo mpya mchakato wa kutafuta amani ambao umekuwa ukisuasua.

 Waasi wa M23 wamefanikiwa kuiteka miji miwili mikubwa mashariki mwa Kongo tangu Januari huku maelfu ya vifo vikiripotiwa na mamia ya maelfu ya watu wakilazimika kuyakimbia makazi yao.

Mapigano hayo yanazidi kupamba moto licha ya juhudi za viongozi  wa nchi za ukanda wa Kusini mwa Mashariki mwa Africa kuutanzua Mgogoro huo unaotishia kusambaa na kuwa vita vikubwa vya kikanda.

Taarifa ya Eric Ponda.  

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version