News
Mnyazi, Awasuta Wanasiasa Wanaoendeleza Siasa za Mgawanyiko
Mbunge wa Malindi Amina Mnyazi amewasuta vikali baadhi ya wanasiasa wanaoendeleza siasa za mgawanyiko, akisema malengo yao ni kuvuruga mipango ya maendeleo kupitia serikali Jumuishi.
Mnyazi amewataka wanasiasa hasa wale waliokuwa ndani ya serikali ya Kenya kwanza na baadaye wakatimuliwa serikalini kutokana na utendakazi wao duni wao kukoma kuendeleza siasa za chuki na migawanyiko.
Mbunge huyo wa Malindi amepongeza juhudi zinazoendelezwa na baadhi ya mawaziri kutoka chama cha ODM walioteuliwa na Rais Ruto kushikilia nyadhfa hizo, akisema ni lazima wakenya waungane ili kufanikisha miradi ya maendeleo.
Wakati huo huo ameweka wazi kwamba siasa za Pwani zinaongozwa na Waziri Hassan Ali Joho, na akiwataka wale wanaolenga kuungwa mkono na wapwani kupitia kwa Joho kwani tayari wapwani wamefanya uamuzi wao kisiasa.