News

Wito wa haki kupatikana watawala mazishi ya Albert Ojwang’

Published

on

Ibada ya mazishi kwa ajili ya mwendazake mwanablogu na mwalimu Albert Ojwang’ aliyeuawa mikononi mwa polisi inafanyika katika shule ya msingi ya Nyawango kaunti ya Homa Bay, huku kukiwa na hali ya taharuki.

Katika hafla hiyo uwepo wa maafisa wa usalama haujashuhudiwa.

Kulingana na Odhiambo Ojiro, mmoja wa wanaharakati katika eneo hilo alisema vijana wamejitolea kumpumzisha Ojwang’ kwa heshima aliyostahili’ na ishara hiyo imeonyesha umoja walionao vijana hao.

Wakizungumza katika hafla hiyo, baadhi ya walimu katika shule ambayo Albert alikuwa akihudumu katika kaunti ya Taita Taveta, wakiongozwa na Ismael Omoke Kongo walishinikiza naibu inspekta jenerali wa Eliud Lagat na wengine waliohusika na mauaji hayo kukamatwa na kufunguliwa mashtaka mahakamani.

Walisema kesi ya mauaji ya dhidi ya Albert inafaa kuchukuliwa kwa uzito na kuharakishwa mahakamani ili haki kwa familia na jamii ipatikane.

“Tunataka hii kesi kuharakishwa na wote waliohusishwa iwe kupitia kutoa maagizo hadi utekelezaji kushtakiwa”, walisema walimu hao

Wanablogu mbali mbali waliofika katika hafla hiyo waliunga mkono kauli ya walimu hao huku wakishikiniza mamlaka ya kutathmini utendakazi wa polisi IPOA na idara ya upelelezi wa makosa ya jinai DCI kuwajibika.

“Yale ambayo mnatenda Mungu anaona, ipo siku sauti zetu zitasikika, mimi naambia IPOA na DCI mnatatiza haki kwa Albert na nataka mmkamate mshtakiwa, na tunaambia serikali huwezi kutuua na utuongoze”, walisema wanablogu.

Ojwang’ alichukuliwa nyumbani kwao kaunti ya Homabay na maafisa wa usalama na kusafirishwa hadi kituo cha polisi cha Central jijini Nairobi ambapo alitangazwa kufariki baadaye.

Wakati huo polisi walitoa taarifa na kudai Albert alifariki baada ya kujigonga kwenye ukuta wa chumba cha seli alimokuwa anazuiliwa kituoni Central.

Mauaji ya Albert yalizua hasira miongoni mwa wakenya hasa vijana wa kizazi cha Gen Z, ambao wamekuwa wakiendeleza misururu ya maandamano nchini.

Taarifa ya Joseph Jira

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version