Entertainment

What Is Nyevu? Magwaya, Deal na Mihangaiko Yako Tafadhali~Kelechi Afrikana

💥 Ujumbe wa mafumbo, mkorogo, na mzaha wa ‘something wet’ waunda kisanga cha kitaa!

Published

on

Msanii maarufu wa R&B kutoka Pwani, Kelechi Afrikana, hatimaye amevunja ukimya wake – lakini si kwa kuachia wimbo. Badala yake, alichagua kujibu post ya muunda maudhui Nyevu Fondo kwa njia ya fumbo lenye uzito wa hisia, ladha ya ucheshi, na dongo lililotupwa kwa ustadi wa kisanaa.

Kwa mtindo wake wa kipekee, aliandika mistari iliyobeba mafumbo mazito lakini yaliyopenya kwa wepesi miongoni mwa mashabiki: “Kuna mshangazi umemshinda Magwaya Ndani. Naona unataka niletea lawama. Magwaya, deal na mihangaiko yako tafadhali.”

Hapo ndipo hali ikaanza kuchacha, na mtandao ukaanza kutafuta maana halisi ya ujumbe huo uliojificha.

Lakini kilichogeuza tahadhari hiyo kuwa kisanga cha mtandao ni fumbo lake lililotangulia: “What is nyevu… Something wet right…” 🤔💧

Ndani ya dakika chache, mitandao ikageuka darasa la kiswahili, maabara ya tafsiri na tamasha la vicheko – kila mtu alikuwa na version yake ya ‘nyevu’! 😂📱

🔸 Amos Tsui Chai

“Nyevuu Fondo ati inamaanisha noni 😅. Msamehe yuyu maana amalacho khondo nacho kinadima kumwika hafufu ela khamanya.”

🔸 Rehma Chikophe

“Anasema wewe na Chikuzeee ni customer wake wa mkorogooo 😂😂😂😂”

Muda huo mashabiki walikuwa tayari wameunganisha dots kuliko DCI – Kelechi, Chikuzee, na mkorogo! 🤣

🔸 Ammigo Dunga

“Namuona NYEVU akiandika na akifuta ila sijakufa moyo, nasubiri comeback yake. Something wet 🤣😂😂😂”

🔸 Bradley Pato

“Ati ‘something wet right?’ We Kelechi ni fala sana. Huwezi mwacha dadako kwa hali hiyo 😂😂😂 unataka ajinyonge??”

🔸 Khadijah Ali

“Kuna watu ni washari hapa duniani eti ‘something wet right’ 🤣🤣🤣🤣🤣”

Ikumbukwe kuwa Nyevu Fondo aliandika kwenye ukurasa wake akisema: “Huyu Kelechi Africana na Chikuzee Kenya tangu niwauzie mkorogo nkama wali-bleach hadi akili 🥱😂”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version