Entertainment

Tuache Wengine Washine, Wito wa Diana B kwa Mashabiki Wake

Published

on

Mwanamuziki wa Kenya, Diana Marua, maarufu kama Diana B, amewataka mashabiki wake kuacha wivu na kushirikiana katika kuusukuma wimbo wake mpya Bibi ya Tajiri hadi kufikisha watazamaji milioni moja kwenye YouTube.

Wito huu aliutoa kupitia ukurasa wake wa Facebook baada ya kufurahia hatua ya kufikisha zaidi ya 700,000 views ndani ya muda mfupi tangu kuachia kibao hicho.

“Cheki Dem 😍😍😍 Kenyans have united once again thanks to #DIANAB 😂😂😂 Don’t be deceived by her looks! She is a Ticking Time Bomb 💣😉 700K+ VIEWS INNIT 🥳 Let’s get #BIBIYATAJIRI to 1M Tuache Wengine Washine Sasa!…,” aliandika Diana.

Wengi walimjua Diana Marua awali kama mke wa msanii Bahati, lakini kupitia jina la kisanii Diana B, ameonyesha kuwa anaweza kusimama peke yake jukwaani.

Alipozindua safari yake ya muziki, alikumbana na kejeli, shaka na ukosoaji mkali. Hata hivyo, nyimbo kama Hatutaachana na One Day zilithibitisha kuwa amejipanga kwa safari ndefu.

Kupitia Bibi ya Tajiri, amedhihirisha uthabiti wake na kutuma ujumbe wa wazi kwamba anapania kushindana na majina makubwa ya muziki nchini kama Otile Brown, Khaligraph Jones na Bahati.

Wimbo huu umegusa hisia za mashabiki kwa jina lake la kipekee na ujumbe wa kijamii unaohusu nafasi ya mwanamke mwenye ushawishi na nguvu za kifedha.
Video yenye rangi kali, miondoko ya kisasa na uchezaji wa kuvutia imechangia zaidi kufanya kibao hiki kuwa gumzo mitandaoni.

Ndani ya siku chache, Bibi ya Tajiri si tu wimbo, bali mjadalawa kitaifa kuhusu nafasi ya wanawake kwenye muziki wa kisasa na jamii ya leo.

Safari ya Diana haiwezi kutenganishwa na msaada wa mumewe, Bahati, ambaye mara kwa mara hujitokeza kumtetea dhidi ya wakosoaji.
Ushirikiano wao umeibua picha ya wanandoa wenye ushawishi mkubwa katika tasnia ya burudani ya Kenya.
Mafanikio ya Bibi ya Tajiri pia ni kielelezo cha ushirikiano wa kifamilia unaochochea sanaa.

Diana ameeleza wazi kuwa changamoto kubwa inayokwamisha sanaa nchini ni wivu na kutoaminiana.
Wito wake wa “Tuache wengine washine sasa” ni mwamko wa kuhimiza mashabiki wa muziki wa Kenya kushirikiana badala ya kudidimiza jitihada za wasanii wa ndani.

Kupitia kampeni za mtandaoni, changamoto za TikTok na mawasiliano ya karibu na mashabiki, Diana amefanikisha hatua kubwa katika kupanua ushawishi wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version