News
Serikali kuwakabili wanyakuzi wa ardhi za shule
Serikali imewaonya watu wanaomiliki mashamba ya shule sawa na wenye nia ya kunyakua ardhi za taasisi za elimu kwamba watakabiliwa kisheria.
Waziri wa elimu Julius Migos Ogamba, alisema serikali imeunda kamati maalum ya kunakili raslimali zote za shule humu nchini, huku wakilenga kutengeneza hatimiliki za shule ili kukabiliana na unyakuzi wa mashamba ya taasisi za elimu.
Akizungumza eneo la Rabai kaunti ya Kilifi, Ogamba alisema ardhi za taasisi za elimu zinalindwa na kwamba wizara yake itawachukulia hatua za kisheria watakaopatikana na makaosa hayo.
Wakati huo huo waziri huyo alifichua kwamba tayari serikali inalenga kuanzisha mpango wa kufadhili chakula katika taasisi husika vile vile kuziunganisha na maji, hasa taasisi zilizoko kwenye maeneo kame.
“Hizi sehemu ambazo ziko na shida ya maji, kuko na shida ya ukame, kuko na shida ya njaa, tunafaa kuja na mikakati dhabiti kuhakikisha hawa wanafunzi tunawainua wafike katika kiwango cha watoto wengine nchini, kwasababu bilka elimu hawatakuwa na ushindani unaotakikana”, alisema Ogamba.
Taarifa ya Mwanahabari wetu