Sports
Vilabu Vinavyoshriki Mashindano Ya CAF Kuvuna Maradufu
Ni Afueni kwa vilabu vya Kenya Police na Nairobi United vinavyowakilisha nchi kwenye mashindano ya kilabu bingwa barani (CAF Champions Ligi) na taji la mashirikisho (CAF Confederation) mtawalia.
Hii ni baada ya shirikisho la soka Barani Afrika CAF kutangaza ongezeko la asilimia 100 ya kipato ambacho vilabu vilikua vinavuna misimu ya nyuma.
vilabu vyote 130 vinatarajiwa kunufaika na ongezeko hilo ambapo vilabu ambavyo vilipokea dolla 50,000 sawa na shilingi milioni 6.4 na ya Kenya sasa vitapokea Dolla Milioni 100,000 sawa na Milioni 12.4 ya Kenya.
Hatua hii mpya iliotangazwa na Rais wa CAF Patrice Motsepe itasaidia pakubwa vilabu katika usafiri na maandalizi kwa ajili ya mashindano hayo kwa jumla.
Kenya inawakilishwa na kenya Police Ligi ya Mabingwa Barani huku Nairobi United wakilisha katika taji la mashirikisho Barani Afrika.