News
Rais Ruto: Wazazi tuchunge watoto wetu
Rais William Ruto amewashauri wazazi kote nchini kuhakikisha wanawalekuza vijana wao katika mazingira ya maadili na uwajibikaji na wala sio kuwasukuma katika maisha ya kuhangaika.
Rais Ruto aliwahimiza wazazi, viongozi wa kisiasa na kidini kuhakikisha vijana wanazingatia maadili mema, kuwapa mazingira bora na kuhakikisha wanajitenga na makundi potovu.
Akizungumza baada ya kuhudhuria Ibada ya Jumapili katika Kanisa ya AIC Bomani katika kaunti ya Maachakos, Kiongozi wa nchi, alihimiza ushirikiano wa viongozi wote nchini ikiwemo wa kidini ili kuhakikisha wanawalida vijana kwani na nguzo kuu ya taifa.
“Watoto wetu ni zawadi kutoka kwa Mungu kwa familia zetu na taifa. Ni lazima tuwaelekeze, uzazi jukumu ulilopewa na Mungu”, tuachie Kanisa au serikali pekee jamani na tusikubali kuruhusu mtoto wako alelewe na wapiti njia”, alisema Rais Ruto.
Wakati huo huo aliwarai viongozi wa kisiasa kutowachochea vijana na kuzua vurugu sawa na kuharibu mali ya umma, akisema ni jukumu la wazazi, viongozi wa kidini na kisiasa kuwaelekeza vijana katika mwongozo bora.
Kauli yake imejiri baada ya taifa kuhushudia baadhi ya vijana wakipoteza maisha yao baada ya kupigwa risasi na maafisa wa polisi wakati wa makabiliana kati ya polisi na waandamanaji katika maeneo mbalimbali ya taifa.
Taarifa ya Mwahoka Mtsumi