Business
Vijana 1,500 wafaidika na mafunzo ya Kilimo,Kwale
Kama njia mojawapo ya kukabiliana na ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana nchini, vijana 1,500 kutoka kaunti ya Kwale wamepokea mafunzo ya miaka miwili ya kilimo cha kisasa.
Mafunzo hayo ya kilimo hai kisichotumia kemikali kimetolewa na shirika la Ripple Effect Kenya likishirikiana na serikali ya Kwale katika maeneo bunge ya Matuga, Msambweni na Lungalunga.
Afisa wa shirika hilo Hamisi Hassan na afisa wa mimea kutoka kaunti ya Kwale Joseph Mutisya walisema kuwa mafunzo hayo yamewapa vijana uwezo na maarifa ya kujitegemea kimaisha kupitia mbinu ya ukulima.
Kwa upande wao baadhi ya vijana wa kaunti hiyo akiwemo Asha Rajab na Mary Ndanu walikiri kufaidika na mafunzo ya ufugaji wa kuku, kilimo cha matunda na mboga.
Tarifa ya Mwanahabari wetu.