Business
Ujenzi wa soko jipya Malindi kuboresha biashara
Idara ya biashara na viwanda kaunti ya kilifi imesema kuwa mpango wa ujenzi wa soko jipya la kisasa mjini Malindi ni hatua itakayopiga jeki sekta ya biashara na kuimarisha uchumi wa eneo hilo.
Afisa wa maswala ya kibiashara eneo la Malindi Emily Jira alisema kuwa takriban wafanyibiashara 200 watapata nafasi ya kutekeleza biashara zao ndani ya soko hilo na katika mazingira bora zaidi.
Jira alidokeza kuwa mradi huo utaiwezesha serikali ya kaunti ya Kilifi kuongeza kiwango cha mapato ya ushuru wa masoko kutokana na ongezeko la idadi ya masoko mjini Malindi.
Aidha Jira aliwasihi wafanyibiashara kulipa ushuru hasa kupitia mfumo wa kisasa wa ulipaji ushuru ili kuiwezesha serikali kuboresha mazingira zaidi ya kibiashara.
Tarifa ya Pauline Mwango.