Sports

Thomas Frank Kocha Mpya Spurs!

Published

on

Kilabu ya Tottenham Hotspurs kumtangaza kocha wa sasa wa Brenford Thomas Frank kuwa kocha mpya wa kilabu hiyo kumrithi Ange Postecoglou aliyepigwa kalamu wiki jana kutokana na msururu wa matokeo duni.

Kulingana na mkali wa taarifa Uhamisho barani Ulaya Fabrizio Romano ni kwamba makubaliano ya pande zote mbili zimafikiwa huku Spurs wakiwa tayari kulipia ada ya pauni milioni 10 ikiwa ni kifungu kilichomo kwenye mkataba wa kocha huyo kabila kukamilisha usajili huo.

Duru za kuaminika zaarifu kwamba mwalimu huyo amekubaliana na kilabu hiyo kwa matakwa ya binafsi na yuko tayari kuanza upya na kilabu hiyo ya London Kaskazini msimu ujao.

Raia huyo wa Uingereza mwenye umri wa miaka 51 aliongoza Brenford kumaliza kumi bora msimu uliopita na alama 56.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version