Sports
Tanzania Kupitia Wizara Ya Michezo Yaanza Hamasa Kwa Mashabiki Kuelekea Chan
Hamasa za mashabiki wa Taifa Stars kuelekea michuano ya CHAN 2024 itakayoanza Agosti 2,2025 rasmi zimezinduliwa leo Julai 22,2025 viwanja vya Mbagala Zakhem.
Taifa la Tanzania kupitia kwa Wizara ya michezo hii leo imeanzisha hamasa za michuano ya Chan ambayo inangoa nanga Agosti 2 ugani Benjamin Mkapa nchini Humu.
Shughuli hiyo kulingana na Waziri msaidizi wa wizara ya Michezo Hamis Mwinjuma ni sehemu ya kurai mashabiki kujitokeza kwa wingi kutazama michuano hiyo na kushabikia vijana wa nyumbani timu ya Taifa Stars.
Taifa hilo linafungua kampeini yake dhidi ya Burkina Faso mechi za kundi B kabila ya kukwaruzana na Mauritania,kisha Madagascar kabila ya kufunga na Central Afrika Republic.