Sports
Tanzania Kupitia Wizara Ya Michezo Yaanza Hamasa Kwa Mashabiki Kuelekea Chan

Hamasa za mashabiki wa Taifa Stars kuelekea michuano ya CHAN 2024 itakayoanza Agosti 2,2025 rasmi zimezinduliwa leo Julai 22,2025 viwanja vya Mbagala Zakhem.
Taifa la Tanzania kupitia kwa Wizara ya michezo hii leo imeanzisha hamasa za michuano ya Chan ambayo inangoa nanga Agosti 2 ugani Benjamin Mkapa nchini Humu.
Shughuli hiyo kulingana na Waziri msaidizi wa wizara ya Michezo Hamis Mwinjuma ni sehemu ya kurai mashabiki kujitokeza kwa wingi kutazama michuano hiyo na kushabikia vijana wa nyumbani timu ya Taifa Stars.
Taifa hilo linafungua kampeini yake dhidi ya Burkina Faso mechi za kundi B kabila ya kukwaruzana na Mauritania,kisha Madagascar kabila ya kufunga na Central Afrika Republic.
Continue Reading
Sports
Kocha Wa Stars Benni McCarthy Atoa Sababu Ya Kujiondoa CECAFA

Mkufunzi wa Timu ya Taifa ya Soka Harambee Stars Benni McCarthy amesema kwamba walienda Tanzania kushiriki Kombe la CECAFA wakiwa na azma na ari kubwa ya kuhahakisha wanajiandaa vyema kwa taji la Chan mwezi Ujao ila mandhari waliokutana nayo hayakua ya kuridhisha ndipo wakafikia makubaliano ya kurejea nchini.
Akizungumza kwa mara ya kwanza vijana wa nyumbani wakizidi kujinoa Ugani Nyayo mwalimu huyo amekiri mortisha iliku juu mno ila mazingira hayo hayangeruhusu wao kufanya Kazi na kujianda Ugani Karatu Arusha. “Tuliketi chini kama benchi la Kiufundi tukaona ubora wa viwanja vya mazoezi na wa michezo tukaona itakua si salama kwa wachezaji kuelekea CHAN hivyo tukarejea”.
Haya yanajiri baada ya stars kujiondoa kwenye kipute Cha CECAFA Cha Mataifa Manne nchini Tanzania siku ya Jumatatu huku maswali chungu nzima yakibaki vinywani mwa wengi.
Hata hivyo mwalimu huyo anasema kwa sasa wanajitayarisha zaidi kwa Kombe Hilo kwani wanajua fika ugumu wa kundi lao.
Stars wako KUNDI A pamoja na Angola, Morocco, Zambia na DR.Congo.
Sports
England Ndaani Ya Fainali EURO Ya Akina Dada

Mabingwa watetezi wa michuano ya kombe la Mataifa ya Ulaya kwa Wanawake #WEURO Uingereza (England) wametinga fainali ya michuano hiyo kwa mwaka 2025, #WEURO2025 kufuatia ushindi wa 2-1 kwenye muda wa ziada wakiifunga Italia kwa mara ya kwanza kihistoria.
England imetangulia fainali kumsuburi mmoja kati ya Uhispania au Ujerumani watakaochuana hii leo kwenye nusu fainali nyingine ya #WEURO2025
FT: England 2-1 Italy
90+6′ Michelle Agyemang
119′ Chloe Kelly
33′ Barbara Bonansea