Entertainment
Lisemwalo Lipo, Apewe Nafasi Afunguke, Kaa la Moto Amkingia Kifua Kelechi Africana
Msanii nguli wa muziki Afrika Mashariki, Kaa la Moto, amekingia kifua kauli ya msanii mwenzake Kelechi Africana aliyedai kuwa “kinachowafelisha wanamuziki wa Mombasa ni ukahaba.”
Akizungumza na meza ya burudani ya Coco FM, Kaa la Moto alieleza kuwa anaamini nia ya Kelechi si ya kubeza bali ya kutaka kuona mabadiliko chanya kwenye tasnia ya muziki kutoka ukanda wa Pwani.
“Ameona ndio maana anayakemea,” alisema Kaa la Moto kwa utulivu.
“Naamini kwamba ana ufahamu sahihi, na pia naamini kuwa ni kijana ambaye anataka maendeleo ya sanaa kutoka mkoa wake. Kwa hiyo watu walipatie fikra—kwa sababu lisemwalo lipo. Labda ana kitu, akipewa nafasi atazungumza zaidi.”
Kauli ya Kelechi ilizua hisia mseto mitandaoni baada ya kupachikwa kwenye ukurasa wake wa Facebook, ambapo aliandika: “Kinacho felisha wanamuziki wa Mombasa ni ukahaba.”
Wengine waliona ni matusi kwa jumuiya ya wasanii, lakini kwa Kaa la Moto, ilikuwa ni hoja yenye mzizi wa ukweli. Alisisitiza kuwa hakuna hoja inayopaswa kupuuzwa kabla ya kueleweka kwa undani.
“Sipingi hoja yake kwa sababu kila hoja ipo huru kwa aliyeifikiria na kuiwaza. Naamini anajaribu kuinspire vijana wenzake,” aliongeza Kelechi.
Katika mazungumzo hayo, Kaa la Moto pia alitumia fursa hiyo kueleza kinachomuweka relevant kwenye muziki licha ya mabadiliko ya ladha, mitindo, na majina mapya kwenye game kila mwaka.
“Kitu ambacho kimeniweka hadi leo ni nidhamu. Nidhamu kwenye maisha, kwenye kazi, kwenye watu,” alisema kwa msisitizo.
Baadhi ya mashabiki waliopena maoni yao kwenye post ya Kelechi walisema;
Tamara Black, “Shida tu unaingililia watu hawana shughuli yako.Put that effort in Use ututolee kazi kali umbea achia watoto wa kike.”
Raisi Wakitaa, “Apo umenena nimepata mwenzangu sasa wakusema ukweli wanaboesha Sana Kwanza uyo my wife ndo kabisa simuelewi kila siku post ya mtu mmoja demu mwenyewe alishaliwa na wahuni toka enzi za shule
D Jay Ricious,”Wapashe adi wagutuke maana tulio chini ni huko juu ndio twaja kwa nafasi zetu. #coast music occupy kenya
Hamza Ahmed Lama, “Acha kutafuta Kiki’kai anapiga hela na anamadili kibao.”
Knasty Snaty, “Wew nawew wataka dera kazi yako ni umbea tu acha mziki uanze umbea.”