Kipa wa Real Thibaut Courtois kukosa kudakia Ubelgiji mechi za kufuzu kombe la Dunia

Kipa wa Real Thibaut Courtois kukosa kudakia Ubelgiji mechi za kufuzu kombe la Dunia

Kipa wa timu ya taifa ya Ubelgiji, Thibaut Courtois, yuko mashakani kucheza mechi za kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Kazakhstan na Liechtenstein baada ya kuumia mguuni wakati akichezea Real Madrid, klabu yake ya Uhispania, Jumatatu.

Courtois, mwenye umri wa miaka 33, alipata jeraha kwenye misuli ya paja (adductor) wakati wa sare tasa ya Madrid dhidi ya Rayo Vallecano kwenye mechi ya La Liga iliyochezwa Jumapili.

Madrid haikutoa muda rasmi wa kuwa nje kwa mchezaji huyo, lakini vyombo vya habari vya Uhispania vimeripoti kwamba atakuwa nje kwa kati ya siku 10 hadi 12. Hivyo basi, Courtois anaweza kurejea kwa mechi ya La Liga dhidi ya Elche tarehe 23 Novemba.

Ubelgiji watapata tiketi ya kufuzu kwa Kombe la Dunia la mwakani endapo watashinda dhidi ya Kazakhstan siku ya Jumamosi.

Watahitimisha kampeni yao ya Kundi J kwa mechi dhidi ya Liechtenstein siku tatu baadaye.