Mbunge wa Kiharu Ndindi Nyoro amesisitiza umuhimu wa serikali kuweka mikakati thabiti itakayohakikisha elimu katika shule za upili za kutwa inatolewa bila malipo.
Akizungumza jijini Mombasa, Nyoro alipendekeza kuanzishwa kwa mfuko maalum wa kitaifa wa kukusanya rasilimali zitakazosaidia kugharamia masomo ya wanafunzi wote katika shule hizo kote nchini.
Kwa mujibu wa mbunge huyo, utekelezaji wa pendekezo hilo utaondoa vikwazo vya kifedha na kuhakikisha kila mtoto wa Kenya anapata haki ya elimu.
Aidha, Nyoro aliwataka viongozi wa kisiasa kuacha kutumia masuala ya elimu kama nyenzo ya kutafuta umaarufu, akiahidi kushiriki kikamilifu katika juhudi za kuhakikisha elimu ya shule za upili za kutwa inakuwa bure kwa wote.
Taarifa ya Mwanahabari wetu
