Rais Ruto amteua Mama Ida Odinga kuwa Balozi na Mwakilishi wa Kenya katika UNEP

Rais Ruto amteua Mama Ida Odinga kuwa Balozi na Mwakilishi wa Kenya katika UNEP

Rais William Ruto amemteua mke wa Hayati Raila Odinga, Mama Ida Odinga kuwa Balozi na Mwakilishi wa kudumu wa Kenya katika Shirika la Mazingira la Umoja wa mataifa UNEP.

Uteuzi wake umetangazwa rasmi na Mkuu wa utumishi wa umma Felix Koskei na kuchapishwa katika gazeti rasmi la serikali.

Koskei amesema rais Ruto ametumia mamlaka yake ya kikatiba na kumteua Mama Ida kushikilia wadhfa huo sawa na kuendeleza juhudi za serikali za kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi, kuendeleza sera za taifa za mazingira pamoja na kuhakikisha umoja wa mataifa uchangia pakubwa utumizi wa mazingira.

Rais Ruto amesifia juhudi zilizofanywa na Mama Ida katika sekta ya elimu, mchapa kazi, na kusimamia na Hayati Raila Odinga katika ulingo wa siasa huku Mama Ida akitarajiwa kufika mbungeni kupigwa msasa kabla ya kuanza majukumu yake mpya.

Uteuzi huo umejiri baada ya Rais Ruto jumahili kufanya mabadiliko kadhaa katika nyadhfa za ubalozi ili kuhakikisha Kenya na mataifa mbalimbali ulimwenguni yanaimarisha uhusiano wao mwema.

Mama Ida inachukua nafasi hiyo baada ya Ababu Namwamba ambae alikuwa akishikilia wadhfa huo kuteuliwa na rais Ruto kama Balozi wa Kenya nchini Uganda.

Taarifa ya Mwanahabari wetu