TIMU ZA KILIFI ZA KARATE ZANGAA SIKU YA KWANZA YA MASHINDANO YA AFRIKA MASHABIKI!  

TIMU ZA KILIFI ZA KARATE ZANGAA SIKU YA KWANZA YA MASHINDANO YA AFRIKA MASHABIKI!  
Rais wa chama cha Karate nchini JKA wakili George ameweza kutambua ubora ulioonyeshwa na timu kutoka Kilifi zinazoshiriki kwenye Toleo la Pili la Mashindano ya Afrika Mashariki ya JKA Karate yanayoendelea katika uwanja wa Nyayo.
JKA–Kilifi Young Eagles Karate Club walitoa ushindani wa kuvutia, wakinyakua jumla ya medali 12: Dhahabu 3, Fedha 5, na Shaba 4. Nidhamu, kujituma, na roho yao ya ushindani vinaendelea kuweka kiwango cha juu kwenye mashindano haya.
JKA–Malindi Tigers pia walionyesha kipaji cha kuvutia, wakishinda medali 2 — Fedha 1 na Shaba 1 — na kuthibitisha uwezo wao kupitia mbinu madhubuti na umoja wa timu katika kila hatua ya mashindano.
JKA–Matsangoni Karate Club nao walitoa mchango wa kupongezwa, wakijinyakulia medali 2 za Fedha, ishara ya kujitolea kwao na dhamira ya kuendelea kukua na kung’ara kwenye mchezo wa karate.
Aidha ameweza kuwapongeza wanariadha wote, makocha, na wadau kwa mafanikio yao makubwa na uwakilishi wa kutia moyo. Bidii na uthabiti wao vinaendelea kuhamasisha na kuinua hadhi ya karate katika ukanda wetu.