Familia za wakenya waliokwama nchini Urusi zinaendelea kulilia serikali kuingilia kati kuwarejeshwa jamaa zao nyumbani.
Baadhi ya wakenya hao wanaripotiwa kuzuiliwa kama wafungwa wa vita na majeshi ya Ukraine huku wengine wakiripoti kuuawa.
Wizara ya mashauri ya kigeni nchini ilisema kuwa wengi wa wanaoripotiwa walisajiliwa kwa njia zisizo halali.
Familia ya Oscar Agola Ojiambo imekuwa ikifanya ziara za mara kwa mara katika ofisi za mashauri za kigeni zilizoko Upper Hill Nairobi kufuatilia na kuiomba serikali iingiliea kati ili kufanikisha kurejeshwa kwa mwili wa mpandwa wao nyumbani.
Ojiambo mwanajeshi wa zamani wa KDF aliondoka nchini mwezi juni mwaka jana 2025 kujiunga na jeshi la Urusi, japo mwezi mmoja baadaye mawasiliano yake na familia yalikatika ghafla na hawajapata habari zozote kumhusu.
Katibu wa mashauri ya kigeni Daktari Korir Sing’oei alisema japo serikali ya kenya imejitolea kuwalinda raia wake walio nje ya nchi, baadhi ya wakenya wamekuwa waathiriwa wa ulanguzi wa binadam.
Taarifa ya Joseph Jira
