MATANO MANE FC
Timu ya soka ya vijana ya Matano Mane ni Moja wapo ya timu zinazo kua Kwa kasi sana kutoka wadi ya Sokoke, Kaunti ndogo ya Ganze – Kilifi.
Ni timu ambayo inatia fora viwanjani sio tu Kwa mashabiki wake kutoka eneo la Matano mane bali kuvutia umaarufu kote katika kaunti ya Kilifi.
Kwa sasa timu hiyo inashiriki ligi ya divesheni ya pili ukanda wa Pwani kaskazini, chini ya ukufunzi wa Emmanuel Mwalugo.
Hivi majuzi timu hiyo ilishiriki katika kombe maalum la CocoFm Super Cup makala ya kwanza yaliyofanyika Jumanne ya Disemba 16 na Jumatano ya Disemba 17 katika uga wa Mmkoroshoni mjini Kilifi.
Kombe hili ambalo lilidhaminiwa moja Kwa moja na kituo cha utangazaji cha Coco fm Kwa ushirikiano na Wakfu wa George Kithi, linalenga kukuza zaidi talanta kutoka nyanjani haswa timu kama hii ya Matano Mane FC.
Kikosi hicho kilianza mashindano hayo kwa kishindo baada ya kuinyuka klabu ya Ubuntu, watani wao wa jadi Kwa magoli 5-4 kupitia mikwaju ya penalti baada ya dakika 90 za sare.
Mshambulizi John Kai ambaye aliibuka na taji la kiatu cha dhahabu, kwa kuwa mfungaji bora zaidi baada ya kufunga wingi wa mabao manne, alitanguliza kwa penalti huku nahodha Pascal Mwalugo, Maura na James Kahindi wote wakifunga penalti zao kwenye ushindi huo
Hata hivyo safari ya vijana hao ilisitishwa na mabingwa wa Kombe hilo Mariakani FC ambao waliwabandua kwa magoli 4-2 kupitia mikwaju ya penalti baada ya sare ya magoli 2-2 muda wa kawaida.
Matano Mane walichukua uongozi wa mapema kupitia Beki na nahodha Pascal Mwalugo dakika ya kwanza ya mchezo kabla ya Mariakani kusawazisha kupitia mshambulizi Ramadhan Mandela kunako dakika ya 17. Mariakani walichukua tena uongozi kupitia mshambulizi James Ndege kabila ya John Kai Piri kusawazisha na kufunga goli la pili dakika ya 69.
Hata hivyo kwenye mikwaju ya penalty Joh Kai Piri alipoteza pamoja na beki Pascal Mwalugo na kuifanya Mariakani kufuzu kwenye fainali nao Matano Nane kucheza kwenye kusaka nafasi ya tatu bora
Katika mechi ya kutafuta mshndi wa tatu kabila ya fainali dhidi ya Mbungoni United, vijana hao walijituma ila bado walisalimu amri licha ya kutoka sare ya magoli 2-2 na kupoteza magoli 5-3 kupitia matuta na kumaliza nafasi ya nne wakiondoka mikono mitupu.
Hii hapa ni kikosi cha Matano Mane mashindano ya Coco fm Supercup;
kikosi cha Matano mane
Magolikipa;
Baraka wanje
Victor Kombe Yeri
Alex Kahindi.
Mabeki;
Pascal Mwalugo (C,)
Kennedy Sammy
Victor Kifalu
James Katana
Alphonce Atieno
Solomon sifa.
Viungo wa Kati;
Shabir Siyra James
Julius Menza
Enock Karima
Jared Uhuru
Michael Mwalugo
Fred Gandi
Masha Charo
Simon Karisa
Erick Piri
Washambulizi;
Hassan James
Abdul Mashanga
Hillan Kesi
Kahindi Menza
John Kai Piri
Kocha:
Emmanuel Mwalugo.
Naibu Kocha:
Erick Menza
Meneja wa Timu;
Onesmas Garam
