News

Spika Mwambire Alalamikia Kucheleweshwa kwa Fedha za Kaunti

Published

on

 

Spika wa bunge la kaunti ya Kilifi Teddy Mwambire amelalamikia hatua ya serikali kuu kuchelewesha usambazaji wa fedha za serikali za kaunti, akidai kwamba hatua hiyo imelemaza utendakazi mashinani.

Mwambire amesema hali hiyo huenda ikachangia idadi ya wafanyakazi ikiwemo maafisa wa mabunge ya kaunti sawa na viongozi wa mabunge hayo kupunguzwa.Aidha amesema licha ya changamoto hiyo, wafanyakazi wa bunge la kaunti ya Kilifi wamekuwa wakitekeleza majukumu yao kwa bidii kwa lengo la kuboresha gatuzi la Kilifi.

Wakati huo huo amesifia bunge la kaunti ya Kilifi akilitaja kama bunge bora zaidi kwani halijahusishwa na matumizi mabaya ya fedha za umma jinsi inavyoshuhudiwa katika mabunge mengine ya kaunti humu nchini.

Kiongozi huyo hata hivyo amesema hali hiyo inadhihirisha wazi kwamba viongozi ndani ya bunge hilo wanalenga zaidi matakwa ya wananchi na wala sio kujinufaisha binafsi.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version