News

Serikali kuwalipia wakenya milioni 1.5 gharama za SHA

Published

on

Serikali inasema itawalipia wakenya milioni 1.5 matozo ya bima ya afya – SHA kuanzia wiki ijayo.

Haya ni kwa mujibu wa rais William Ruto ambaye alisema kuwa watakaofaidika na mpango huo ni wale ambao hawana uwezo wa kulipia bima ya afya SHA.

Aidha rais Ruto alisema atafanya mkutano na magavana na wabunge ili wao pia wawalipie pesa hizo wakenya wengine milioni moja.

Kiongozi wa taifa aliongeza kwamba hatua hiyo inalenga kuwawezesha wakenya wote kupata matibabu bila malipo.

Wakati huo huo serikali iliahirisha mpango wa kuwahamisha zaidi ya wafanyakazi 7,400 wa huduma za afya kwa wote (UHC) hadi mwaka ujao 2026.

Aidha wizara ya afya itaendelea kuwalipa mishahara wahudumu hao katika muda huo ambapo watakuwa kwenye mpango wa ajira ya kudumu na yenye pensheni hadi mwezi Juni mwaka ujao.

Haya yameafikiwa baada ya mazungumzo ya kina kati ya waziri wa afya Aden Duale na baraza la magavana.

Taarifa ya Joseph Jira

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version